Rubara Marando, mgombea wa Mwenyekiti wa Taifa wa TAMICO, pamoja na Lucas Bujashi, Katibu Mkuu
Uadilifu,
uwajibikaji
na matokeo.
Chama chetu kinastahili kuwa na nguvu zaidi, kuonekana zaidi, na kuleta matokeo yanayogusa maisha ya kila mwanachama, kazini na nyumbani.
Dhamira yangu
Kutetea haki, maslahi na ustawi wa wanachama kupitia majadiliano yenye ushahidi, uongozi shirikishi, matumizi ya teknolojia, na uzingatiaji kamili wa Katiba na Kanuni za chama.
Misingi ya uongozi wangu
- Uwazi
- Taarifa za utendaji kazi wa chama kwa kila robo.
- Ushirikishwaji
- Maamuzi kufanywa na vyombo vyenye dhamana katika ngazi husika.
- Uwajibikaji
- Ahadi zitapimwa kwa viashiria vinavyopimika.
- Uadilifu
- Katiba na Kanuni ndizo dira ya kila hatua.
- Matokeo
- Kipimo cha uongozi ni maisha bora ya mwanachama.
Uzoefu ndani ya chama
Kazini na kitaaluma
Ahadi zangu nane
Gusa ahadi yoyote kuona maelezo yake kamili.
-
- Kujadiliana na kusaini Mikataba ya Hali Bora (CBAs) katika kila taasisi yenye wanachama.
- Kufuatilia utekelezaji wa mikataba iliyosainiwa, si kuisaini tu.
- Kujadiliana na waajiri kuweka ruzuku bima ya NHIF ili kupanua wigo wa huduma kwa watumishi.
- Kudai motisha (Incentives) kwa watumishi ili kuongeza ari ya utendaji.
-
- Dawati la msaada wa kisheria kwa migogoro ya kikazi, kufukuzwa kazi na makosa ya kinidhamu.
- Kuwawakilisha wanachama katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) na Mahakama ya Kazi.
-
- Mafunzo ya sheria za kazi, haki za mfanyakazi na majadiliano kwa viongozi wa matawi.
- Kuhakikisha taasisi zinaandaa semina za maandalizi ya kustaafu na usimamizi wa fedha binafsi.
- Kuandaa viongozi chipukizi kwa uongozi wa baadaye.
-
- Kuandaa na kuidhinisha Scheme of Service kwa watendaji wa chama.
- Maboresho ya mishahara na stahiki zinazoendana na gharama za maisha.
- Mafunzo endelevu na mazingira bora ya kazi.
- Tathmini ya utendaji iliyo wazi na motisha kwa wanaofanya vizuri.
-
- Nguvu ya chama ni idadi ya wanachama. Bila wingi hatuna sauti mezani.
- Kubaini maeneo mapya ya waajiri.
- Kampeni maalum ya usajili katika taasisi zisizo na matawi.
- Kufufua matawi yaliyolala na kuyapa mafunzo ya uongozi na nyenzo za kazi.
-
- Chama kinapaswa kuwa karibu na makao makuu ya Serikali.
- Kutumia ujuzi wa wanachama kuandaa nyaraka za ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu, Dodoma.
- Kuanza ujenzi wa Ofisi ya Makao Makuu mwaka 2027.
- Jengo litajumuisha miradi ya kuingiza mapato.
-
- Kanzidata (database) ya wanachama yenye usajili mtandaoni na kadi za kidigitali.
- Uwasilishaji wa taarifa za utendaji kupitia mtandao.
- Usambazaji wa jarida (Newsletter) kwa wanachama kila robo mwaka.
- Utwaaji na uwasilishaji wa fomu za kugombea mtandaoni.
-
- Kusimamia uzingatiaji kamili wa Katiba na Kanuni katika chaguzi, vikao na matumizi ya fedha.
- Kuhakikisha vikao vya kikatiba vinafanyika kwa wakati na kumbukumbu zinatunzwa.
- Uwakilishi halisi wa wanawake, vijana, watu wenye ulemavu na kada mbalimbali katika vikao vya maamuzi.
- Kuimarisha kamati za wanawake na vijana kwa bajeti na majukumu ya wazi.
Siku 100 siku za kwanza
- Kukutana na viongozi wa matawi yote na makundi maalum kusikiliza vipaumbele vyao.
- Kufanya tathmini ya hali ya fedha, mali na madeni ya chama, na kuitoa kwa wanachama.
- Kuorodhesha taasisi zisizo na matawi na kuzindua kampeni ya usajili.
- Kuorodhesha mikataba ya hali bora iliyopo, iliyokwisha muda na inayohitajika.
- Kuunda kamati ya mradi wa Makao Makuu Dodoma na kuanza mchakato wa ujenzi.
- Kuanza ujenzi wa kanzidata ya kidigitali ya wanachama.
- Kuzindua dawati la malalamiko na msaada wa kisheria.
Jinsi mtakavyonipima
Kila ahadi itakuwa na kiashiria kinachopimika, na taarifa ya utekelezaji itawasilishwa kila mwaka mbele ya Mkutano Mkuu.
- Wanachama na matawiMiaka 2
Ongezeko la wanachama kwa 30% na matawi mapya katika taasisi zisizo na matawi
- Mikataba ya Hali BoraMiaka 3
Kila tawi kuwa na CBA hai iliyosainiwa
- Makao Makuu DodomaMiaka 3
Kujengwa ofisi za makao makuu
- Scheme of ServiceMwaka 1
Scheme of Service ya watendaji kuidhinishwa na kuanza kutumika
- Bima ya afya na motishaMiaka 2
Makubaliano mapya ya maboresho na waajiri
- Mifumo ya kidigitaliMwaka 1
Wanachama wote kusajiliwa kwenye kanzidata; kadi za kidigitali
- Katiba na KanuniKila mwaka
Vikao vyote vya kikatiba kufanyika kwa wakati
- UshirikishwajiMwaka 1
Makundi maalum kuwakilishwa katika kila kikao cha maamuzi
- Uwazi wa fedhaKila robo
Taarifa za fedha kila robo mwaka; ukaguzi wa nje kila mwaka
- Maoni, malalamiko na maswaliMiezi 6
Mfumo kufanya kazi; angalau 90% ya hoja kujibiwa ndani ya siku 14
Eti Umeonewa na Hausikilizwi?
Kataa WAHUNI!! Kila mwanachama ana haki ya kusikilizwa na kujibiwa. Wakili wa TAMICO ni WAKWAKO! Nita muelekeza
- 1ImepokelewaKukiri ndani ya siku 3
- 2Inashughulikiwa
- 3ImejibiwaJibu kamili ndani ya siku 14
- 4Imefungwa
- Namba ya ufuatiliaji
- Kila hoja inapata namba ya kumbukumbu ili mwanachama afuatilie hatua yake.
- Usiri na ulinzi
- Hakuna mwanachama wala mtendaji atakayeadhibiwa kwa kutoa maoni au lawama.
- Ripoti ya wazi
- Idadi ya hoja zilizopokelewa na kujibiwa itatolewa kila robo mwaka.
Nipeni
kura zenu
Chama hiki ni chetu sote. Nipeni kura zenu za NDIO: tulinde haki zetu, tuboreshe maslahi yetu, tujenge chama chetu.
Chama imara,
mwanachama salama.
Pamoja tunajenga!